History : BeninBenin
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jamhuri ya Benin ni nchi katika Afrika ya Magharibi. Zamani iliitwa Dahomey. Inapakana na Bahari ya Atlantiki upande wa Kusini, nchi ya Togo upande wa Magharibi, nchi ya Nigeria upande wa Mashariki na nchi za Burkina Faso na Niger upande wa Kaskazini. Haihusiani na Mji wa Benin (Benin City) wala na Ufalme wa Benin wa karne ya 19.
- HistoriaUfalme wa Dahomey ulianzishwa katika nchi ya kisasa ya Benin. Katika karne ya 17, ufalme huo uliotawaliwa na oba (ni cheo cha mfalme wake) ulienea sehemu kubwa ya Afrika ya Magharibi. Kulikuwa na utajiri mkubwa kwa sababu ya biashara na Wazungu, hasa Wareno na Waholanzi waliofika kuanzia mwisha wa karne ya 15. Pwani ya Benin ilijulikana kama Pwani ya Watumwa. Biashara ya watumwa iliendelea kwa karne tatu mpaka mwaka wa 1885. Kuanzia karne ya 18, ufalme wa Dahomey ulidhoofika mpaka Ufaransa uliweza kuuvamia mwaka wa 1892. Dahomey ikawa chini ya ukoloni wa Ufaransa kuanzia mwaka wa 1899, na walipata uhuru 1 Agosti, 1960. Mpaka mwaka wa 1972 makundi mbalimbali walipigania vita, mpaka Wakomunisti walianza kutawala na kiongozi wao Mathieu Kérékou. Nchi ilipewa jina lipya, yaani Jamhuri ya Benin, mwaka wa 1975. Tangu miaka ya 80 ya karne ya 20, nchi ilifuata mfumo wa soko huru. Kérékou alikuwa Rais hadi 1991, halafu tena 1996-2006. Katika uchaguzi wa Machi 2006, Yayi Boni alipata urais aliouanza 6 Aprili 2006.
- SiasaTemplate:Siasa ya Benin Bunge la Benin lina viti 83. Huchaguliwa kila mwaka wa nne. Rais ni mkuu wa serikali na wa nchi, naye huchaguliwa kila mwaka wa tano. Mgombea urais asiwe na umri wa miaka zaidi ya sabini.
- UtawalaKuna majimbo 12, nayo ni:
- JiografiaNchi ya Benin iko kati ya Mto wa Niger upande wa Kaskazini na Bahari ya Atlantiki upande wa Kusini. Haina milima mirefu. Idadi kubwa ya watu wanaishi katika tambarare za Kusini ambapo miji mikubwa ya Benin iko, pamoja na miji ya Porto Novo na Cotonou. Sehemu za Kaskazini ni kavu hasa. Nchi ya Benin inapata majira mawili ya mvua, Aprili-Julai na Septemba-Novemba. Pia kuanzia mwezi wa Desemba, kuna upepo ulioitwa harmattan, nao huleta vumbi na baridi wakati wa usiku.
- UchumiUchumi wa Benin hauna nguvu sana, na hutegemea hasa kilimo, mazao ya pamba na biashara ndogondogo.
- Demografia
Kuna makabila mbalimbali ambo wanaongea lugha tofauti sana, k.m. Kihausa, lugha za Kisonghay, lugha za Kimande na lugha za Kifulani. Kabila kubwa kabisa ni Wafon.
- Marejeo
- Viungo ya nje
Categories: Benin | Nchi za Afrika |
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
News
Photo
History
Site
france
espana
Türkiye
Oran
alger
mostaganem
tenes
cherchell
algérie
algérie
algerie
mostaganem
CV